Deriv MT5 signals
Huduma ya biashara ya MT5 signals (ishara) inakuruhusu wewe kujisajili na kunakili biashara za wafanyabiashara wazoefu au kutoa mikakati yako kwa wafanyabiashara wengine kwa ada ya usajili.
Nakili biashara za wataalamu moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Deriv MT5 bure au kwa ada. Mara tu unapojisajili kupata signals (ishara) ya biashara, mikataba ya mtoa huduma itaigwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya biashara ya Deriv MT5 kila mara watakapo fanya biashara.
Faida za kujisajili kwenye ishara za biashara ya MT5
Punguza hatari ya biashara kwa kunakili biashara kutoka kwa wafanyabiashara wabobevu.
Okoa muda – jisajili kupata ishara ili kufanya biashara otomatiki.
Rahisi kusanidi - hakuna usakinishaji unaohitajika.
Ufichuzi kamili wa utendaji wa kila mtoa huduma.
Hakuna magawio wala ada zinazofichwa.

1. Nenda kwenye MQL5 Signals
Katika terminal yako ya biashara ya MT5, nenda kwenye Zana na uchague MQL5 Signals.

2. Jisajili kwa mtoa huduma za ishara
Chagua mtoa ishara unaependelea na bonyeza “Jisajili”.

3. Maliza usajili wako
Panga vigezo vyako vya biashara na udhibiti wa hatari. Kisha bonyeza “SAWA” kukamilisha usajili.
Jinsi ya kurejesha au kughairi usajili wako

1. Nenda kwenye Takwimu Zangu
Katika paneli ya Navigator, nenda kwenye Ishara na bonyeza ‘Takwimu Zangu’.

2. Chagua mtoa huduma
Chagua mtoa huduma za signal (ishara) unayemtaka kuhuisha au kufuta usajili wako.

3. Huisha au jiondoe
Bofya ”Huisha” au “Jiondoe” ili kufufua au kughairi usajili wako.
FAQs
Inagharimu kiasi gani kujisajili ili kupata ishara za MT5?
Jinsi gani naweza kuchagua mtoa huduma wa ishara anayeaminika?
Ikiwa wewe ni mfanyabiashara mtaalamu, shiriki mikakati yako na wafanyabiashara wengine bure au kupitia mpango wa usajili. Wakati wafanyabiashara wanaposajili kupata ishara yako ya biashara, biashara zako zinaigwa moja kwa moja kwenye akaunti zao kila wakati unapoweka biashara.
Faida za kuwa mtoa ishara za biashara ya MT5
Rahisi kusanidi - hakuna usakinishaji unaohitajika.
Kipato cha ziada kutokana na usajili wa kila mwezi.
Okoa muda – biashara zinaigwa moja kwa moja kwenye akaunti za wasajiliwa wako.
Jinsi ya kuwa mtoa (signal) ishara za biashara

1. Jisajili kama muuzaji
Ingia kwenye akaunti yako ya MQL5. Katika ukurasa wa ishara, bonyeza ‘Jisajili’ na ufuate hizi hatua.

2. Ongeza ishara
Bonyeza “Unda ishara” na kamilisha fomu kwa kutumia taarifa za akaunti yako ya Deriv MT5.

3. Simamia ishara (signal)
Nenda sehemu ya ‘Ishara Zangu’ ili kusimamia ishara zako.