Masharti ya jumla
Toleo:
R25|04
Ilisasishwa mara ya mwisho tarehe:
July 2, 2025
Jedwali la yaliyomo
1. Utangulizi
1.1. Kampuni ya Deriv group ni moja wapo ya kundi la zamani lenye mafanikio zaidi ya biashara ya mtandaoni ulimwenguni. Dhamira yetu ya kuzingatia viwango vya juu vya maadili ni mojawapo ya mambo muhimu yatakayohakikisha mafanikio yetu ya kudumu. Kanuni zetu za biashara zinaelezea kwa kifupi maadili yanayoongoza kazi zetu.
1.2. Masharti na vigezo haya yanakuhusu wewe kama Mbia wetu wa Biashara (kama ilivyofafanuliwa katika Kifungu cha 2 hapa chini).
1.3. Ikiwa wewe ni Mshirika, Mtumiaji wa API, Mshiriki wa Programu ya Bug Bounty, na/au Wakala wa Malipo, mhusika wako ni Deriv (SVG) LLC, kampuni iliyoanzishwa katika Saint Vincent na Grenadines, yenye namba ya kampuni 273 LLC 2020.
1.4. Iwapo wewe ni Broker Mwakilishi, upande unaoingia nawe mkataba (kuhusiana na kila mteja aliyealikwa) ni taasisi ambayo mteja aliyealikwa amesajiliwa nayo na kufungua akaunti yake ya biashara, ambayo inaweza kuwa mojawapo ya zifuatazo:
1.4.1. Deriv (FX) Ltd, kampuni iliyoanzishwa Labuan, Malaysia, yenye namba ya kampuni LL13394;
1.4.2. Deriv (BVI) Ltd, kampuni iliyoanzishwa British Virgin Islands, yenye namba ya kampuni 1841206;
1.4.3. Deriv (V) Ltd, kampuni iliyoanzishwa Vanuatu, yenye namba ya kampuni 14556; au
1.4.4. Deriv (SVG) LLC.
1.5. Maneno “sisi”, “sote”, na “yetu” yanarejelea upande wako wa mkataba.
1.6. Vigezo na masharti haya, pamoja na Masharti ya Ziada yanayokuhusu kulingana na kama wewe ni Affiliate (Mshirika), Mtumiaji wa API, Mshiriki wa Bug Bounty Program, Broker Mwakilishi, na/au Wakala wa Malipo, kama yanavyofanyiwa maboresho mara kwa mara, kwa pamoja yatatajwa kama “Masharti ya Biashara”. Iwapo kutakuwa na kutofautiana au kupingana kati ya Masharti haya ya Jumla na Masharti ya Ziada, basi Masharti ya Ziada yatapewa kipaumbele.
1.7. Tutaamua, kwa hiari yetu kabisa, ikiwa maombi yako ya kuwa Mbia wa Biashara yamefanikiwa. Tutakujulisha ikiwa maombi yako yameidhinishwa. Uamuzi wetu ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa.
1.8. Kwa kuwa Mbia wetu wa Biashara, unathibitisha kuwa unakubali na unakubaliana kufuata Masharti haya ya Biashara.
1.9. Kwa kuwa mbia wa biashara, unathibitisha kuwa una umri wa miaka 18 au zaidi. Akaunti za wabia zilizosajiliwa na watu walio chini ya umri huu zitachukuliwa kuwa zimekiuka Masharti haya ya Biashara. Katika kesi kama hizo, tuna haki ya kusitisha mkataba wa ushirikiano mara moja bila taarifa, kufuta gawio zozote ambazo bado hazijalipwa, na kuchukua hatua zozote za ziada zinazohitajika.
1.10. Unawajibika kuangalia tovuti yetu mara kwa mara ili kukagua toleo la sasa la Masharti ya Biashara. Tuna haki ya kufanya maboresho ya Masharti ya Biashara bila kutoa taarifa, na ni jukumu lako kukagua tovuti yetu ili kuona toleo jipya la Masharti ya Biashara. Masharti ya Biashara yaliyofanyiwa maboresho yatakuwa halali mara tu yatakapochapishwa kwenye ukurasa huu. Iwapo utakataa mabadiliko yoyote katika Masharti ya Biashara, ni lazima utujulishe, na tutasitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe kulingana na Kifungu cha 11. Kuendelea kwako kuwa Mbia wetu wa Biashara kutachukuliwa kuwa umekubali mabadiliko hayo.
1.11. Maneno yaliyotumika katika Masharti haya ya Biashara, kama vile “ikiwemo” au “kwa mfano”, si maneno ya kikomo na yatatafsiriwa kama yanavyofuatiwa na maneno “bila kikomo”. Vichwa vya habari katika Masharti haya ya Biashara ni kwa ajili ya urahisi tu na havitaathiri kwa namna yoyote maana au tafsiri ya Masharti ya Biashara.
2. Ufafanuzi
2.1. Mshirika (Affiliate): Chombo au mtu anayetangaza bidhaa na huduma za Deriv kwa malipo ya gawio kulingana na miamala ya wateja walioalikwa kwenye Deriv Trader, Deriv Bot, Deriv GO, SmartTrader, na/au programu za wahusika wengine zinazotumia Deriv API.
2.2. Mtumiaji wa API: Chombo au mtu anayeshirikiana na kiolesura cha programu cha Deriv (API) kupata na kutumia utendakazi na/au data yake ili kujenga programu za biashara za kawaida zinazoshirikiana na majukwaa ya biashara ya Deriv;
2.3. Mbia wa Biashara: Mshirika (Affiliate), Mtumiaji wa API, Mshiriki wa Bug Bounty Program, Broker Mwakilishi, na/au Wakala wa Malipo;
2.4. Mshiriki wa Programu ya Bug Bounty: Mtu ambaye amesajiliwa kushiriki katika programu ya Deriv bug bounty, ambapo unahamasisha washiriki kugundua na kuripoti udhaifu au hitilafu katika mfumo wa programu au mitandao ya Deriv kwa malipo ya fedha, ambapo kiasi cha malipo hayo kitaamuliwa kwa hiari yetu;
2.5. Deriv: Chapa ya “Deriv” na/au jina la biashara;
2.6. Broker Mwakilishi: Chombo au mtu anayetangaza bidhaa za Deriv kwa malipo ya gawio kulingana na miamala ya wateja walioalikwa kwenye Deriv MT5, Deriv X, na/au Deriv cTrader
2.7. Wakala wa Malipo: Mtu binafsi au chombo kinachowezesha uhamishaji wa fedha au malipo kati ya wateja na taasisi ya kifedha au mtoa huduma ya malipo.
3. Kanuni za maadili
3.1. Jumla
3.1.1. Unakubali kwamba utafanya biashara zako kulingana na kanuni zetu. Iwapo hutaki au huwezi kufata kanuni zetu, tuna haki ya kujiondoa katika uhusiano wa kibiashara.
3.1.2. Hupaswi kushiriki katika shughuli zozote, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, ambazo zinaweza kuonekana kwa msingi wowote kuwa zinaharibu sifa ya Deriv.
3.1.3. Hupaswi kamwe kuwaelekeza wateja kwetu ukiwa na maarifa, au kwa matarajio ya msingi, kwamba wateja hao watajihusisha na shughuli za kiuhalifu au zenye nia mbaya (ikiwemo udanganyifu wa mifumo yetu na biashara kwa njia yoyote ile ambayo inaweza kusababisha hasara au madhara yoyote kwa kampuni yetu, yakiwemo madhara ya moja kwa moja, yasiyo ya moja kwa moja, ya kipekee, ya adhabu au ya uharibifu kwetu).
3.2. Uzingatiaji wa sheria na udhibiti
3.2.1. Unawajibika kuhakikisha kuwa unatii sheria, kanuni, na taratibu zote zinazohusika katika nchi unazofanyia shughuli zako. Hizi zinajumuisha sheria zinazohusiana na matangazo, ulinzi wa data, faragha, na uwajibikaji kwa jamii, miongoni mwa mengine.
3.2.2. Iwapo kutakuwa na masuala yoyote ambayo tunaona ni muhimu wateja kufahamishwa ili kuhakikisha uzingatiaji wa mahitaji yoyote ya kisheria au ya kikanuni, au kwa sababu nyingine yoyote, unakubaliana kuwafahamisha haraka wateja wote unaowatambulisha kwetu kuhusu masuala hayo kulingana na maelekezo yetu.
3.3. Biashara inayowajibika
3.3.1. Unapaswa kuhamasisha waalikwa kutoka kwako kutumia akaunti ya demo ili kujijengea ujuzi wao kwa kujaribu bidhaa husika za Deriv bila malipo, badala ya kuanza kufanya biashara kwa kutumia fedha halisi moja kwa moja.
3.3.2. Lazima uwasaidie wateja kupata uelewa wa wazi kuhusu hatari zinazohusiana na bidhaa na huduma zetu. Utawaeleza kwamba hakuna hakikisho la ushindi kamwe, biashara inaweza kuleta uraibu, na wanapaswa kufanya biashara tu kwa kutumia fedha ambazo wako tayari kupoteza, na kamwe wasitumie fedha za kukopa. Wanapaswa kuweka kikomo cha ushindi wao na kamwe wasifanye biashara wakiwa wamechoka au wakiwa chini ya athari za pombe au dawa.
3.3.3. Unaruhusiwa kutoa tu taarifa za kiufundi na kielimu kwa wateja au wateja watarajiwa, na kamwe hupaswi kuwapa aina yoyote ya ushauri wa kifedha, uwekezaji, au wa biashara.
3.3.4. Hupaswi kuhamasisha mteja yeyote unayemtambulisha kwetu kuchukua aina yoyote ya mkopo kwa ajili ya kuweka pesa na/au kufanya biashara.
3.3.5. Hupaswi kutoa au kuahidi kuwapa upatikanaji wa mtaji au fedha wateja ili wafanye biashara nasi.
3.3.6. Hupaswi kuruhusu wateja au wahusika wengine wowote kufikia au kutumia akaunti yoyote ya Deriv uliyounda.
3.4. Uwazi
3.4.1. Taarifa au nyenzo zozote unazowapa wateja, ikijumuisha maelezo kuhusu biashara, Mikataba ya Tofauti (Contracts for Difference), Chaguzi (Options), au maelezo mengine ya bidhaa na huduma tunazotoa, zinapaswa kuwa za kina, zisizo na upendeleo, wazi, na zisizo na vipengele vya kupotosha kwa njia yoyote ile, na pia zizingatie masharti yote yaliyowekwa katika Masharti ya Biashara.
3.5. Hakuna rushwa
3.5.1. Unakubalia kufuata kikamilifu Sera yetu ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi katika kipindi chote cha uhusiano wa kibiashara. Kuwajibika huku kunajumuisha kuepuka kutoa, kupokea, au kuomba aina yoyote ya rushwa, malipo ya siri, malipo yasiyo halali na/au manufaa ya aina nyingine, pamoja na kudumisha uwazi na maadili mema ya kibiashara wakati wote. Kujihusisha na aina zote za rushwa ni marufuku, ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa kwa au kupokea rushwa kutoka kwa maafisa wa serikali au watu wowote au taasisi zilizo katika nafasi za uwajibikaji katika sekta binafsi.
3.5.2. Tuna haki ya kufuatilia na kuthibitisha utekelezaji wako wa Sera ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi. Iwapo utakiuka sera hii, tunaweza kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe bila taarifa, na ukiukaji huo unaweza kusababisha kuchukuliwa kwa hatua za kisheria.
3.6. Kupambana na utakatishaji pesa.
3.6.1. Haturuhusu bidhaa zetu au huduma za malipo zitumike kuwezesha utakatishaji wa fedha, ufadhili wa ugaidi, au shughuli nyingine zozote za kihalifu.
3.6.2. Iwapo utahisi kwamba mteja anatumia fedha zilizopatikana kwa njia isiyo halali, unapaswa kutujulisha kupitia [email protected] haraka iwezekanavyo. Katika kesi kama hizo, tunaweza kuamua kufanya ukaguzi kuhusu hali na historia ya mteja.
3.6.3. Kwa ombi letu, unahitajika kufanya ukaguzi wa Mjue Mteja Wako (KYC) kwa wateja wako kulingana na maelekezo yetu.
3.6.4. Unahitajika kuwafahamisha wateja wanaofanya kazi katika sekta ya benki na/au fedha kwamba hawawezi kufanya biashara kupitia tovuti yetu bila kujulisha waajiri wao. Lazima wahakikishe kuwa biashara yoyote ya aina hiyo inazingatia sera za mwajiri wao.
3.6.5. Lazima uhakikishe kwamba wateja wote watarajiwa wanajua kwamba tumepiga marufuku aina zote za biashara zinazomuhusisha mtu wa ndani (mwajiriwa wa Deriv). Hii inamaanisha kwamba wateja hawaruhusiwi kufanya biashara kwa kutumia taarifa za ndani au maarifa ambayo hayajachapishwa kwa umma. Maarifa kama hayo yanaweza kujumuisha, kwa mfano, taarifa za siri walizopata kupitia kazi zao. Iwapo utakuwa na mashaka yoyote kwamba biashara ya aina hiyo inafanyika, unapaswa kutoa taarifa kupitia [email protected] haraka iwezekanavyo.
3.6.6. Tuna haki ya kusitisha, kuzuia, au kufuta akaunti yoyote ambayo inashukiwa kutumika katika utakatishaji wa pesa.
3.7. Migogoro ya maslahi
3.7.1. Lazima uepuke migogoro ya maslahi. Kwa mfano, hupaswi kushindana nasi, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, wala kutumia maarifa unayopata kutokana na uhusiano wako nasi kusaidia mtu mwingine kushindana nasi.
3.7.2. Iwapo kutatokea mgogoro wa maslahi au unaoweza kutokea wakati wa kazi yako, ni lazima uripoti kwa [email protected] haraka iwezekanavyo.
3.8. Vitabu na rekodi
3.8.1. Lazima uhakikishe kuwa umejaza rekodi zote zinazoakisi miamala yako ya kibiashara kwa usahihi na kwa maelezo yote yanayohitajika.
3.9. Kufichua maovu (Whistleblowing)
3.9.1. Unakubali kuzingatia kikamilifu Sera Yetu ya Kufichua Maovu kwa Wabia katika kipindi chote cha uhusiano wako wa kibiashara nasi. Hii inajumuisha kuripoti mara moja vitendo vyovyote vya ukiukaji, tabia zisizo za kimaadili, uvunjaji wa sheria, au ukiukaji wa sera za kampuni zinazoweza kutokea kuhusiana na shughuli zako. Tunakuhimiza utoe wasiwasi wa aina hiyo kwa nia njema kwa kutuma barua pepe kwa Afisa wa Kufichua Maovu wa Kikundi kupitia [email protected]. Ripoti yako itashughulikiwa kwa usiri na kwa kuzingatia taratibu zetu za uchunguzi wa ndani. Kwa kuzungumza wazi, unatusaidia kudumisha utamaduni wa uwazi, uadilifu, na uwajibikaji.
4. Mfahamu Mbia wako wa Biashara
4.1. Tunaweza kuhitaji utupatie uthibitisho wa utambulisho, uthibitisho wa anwani, na/au hati au taarifa nyingine kuhusu utambulisho wako au masuala ya biashara yako unapowasilisha ombi la kuwa Mbia wa Biashara au katika hatua ijayo, ili tuweze kufanya ukaguzi wetu wa kina (kama sehemu ya udhibiti wa hatari na sifa yetu, pamoja na kutimiza wajibu wetu wa kisheria na wa kikanuni). Unakubali pia kutupatia taarifa na hati zote kuhusu shughuli zako na uwezo wako tunazoweza kuomba mara kwa mara (ambazo zinaweza kuhusiana, kwa mfano, na usajili wako, usajili wa kisheria, uanachama, idhini, maarifa, utaalamu, na/au uzoefu).
4.2. Unakubali na kutambua kwamba iwapo utashindwa kutoa taarifa yoyote inayohitajika wakati wa mchakato wako wa kujiunga kama Mbia wa Biashara, au ikiwa taarifa yoyote uliyotupatia itabainika kuwa si sahihi, haijakamilika, ya udanganyifu, na/au si ya kweli, tuna haki ya kukataa ombi lako, kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe bila taarifa ya awali, na/au kushikilia fedha zozote ulizonazo kwetu.
4.3. Ikiwa taarifa ulizowasilisha wakati wa mchakato wa kujisajili zitabadilika kwa njia yoyote ile wakati wowote, ni lazima utuarifu kupitia barua pepe mara moja.
4.4. Iwapo, kwa sababu yoyote ile, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa idhini, maarifa, utaalamu, uzoefu, au muda, huna tena idhini, uwezo, sifa, au uhitaji wa kutekeleza majukumu na wajibu wowote unaotakiwa kulingana na Masharti haya ya Biashara, ni lazima utuarifu kupitia barua pepe mara moja.
4.5. Baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibiashara, tunaweza kuomba utupatie taarifa za hivi karibuni na/au za ziada ili kumbukumbu zetu za uchunguzi wa kina ziweze kusasishwa ipasavyo. Iwapo utashindwa kutupatia taarifa zinazohitajika ndani ya muda uliowekwa, tuna haki ya kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe bila kutoa taarifa. Fedha zozote ulizonazo kwetu zitalipwa kwako kupitia maelezo ya benki tuliyo nayo kwenye faili, na akaunti yako (au akaunti zako) zitafungwa.
4.6. Tuna haki ya kukataa taarifa zozote unazotoa ambazo zinaonekana kutokuwa za sasa, sahihi, au kamili, au kuomba uthibitishe au kusahihisha maelezo yoyote uliyotoa. Iwapo taarifa unazotoa hazitakidhi mahitaji yetu ya uthibitishaji, tuna haki ya kukataa maombi yako au kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe (kama inavyofaa). Tunaweza pia kushikilia fedha zozote ambazo unazo kwetu.
4.7. Fedha zozote tunazoshuku au tunazoona kuwa zimetokana na shughuli za kihalifu hazitakubaliwa.
5. Haki miliki, masoko, na matangazo
5.1. Hupaswi kamwe kuandaa au kuchapisha maudhui yoyote au kuweka matangazo yoyote yanayotutaja sisi au uhusiano wako nasi bila idhini yetu ya awali ya maandishi.
5.2. Iwapo unamiliki au unaendesha tovuti yoyote ambayo unataka kutaja bidhaa au huduma zetu, utafanya hivyo tu kwa idhini yetu ya awali ya maandishi. Pia utatakiwa kuweka kiunganishi cha tovuti kutoka tovuti yako kwenda tovuti yetu.
5.3. Tunaweza kukutumia nyenzo za masoko na mali mbalimbali za chapa, ikiwa ni pamoja na nakala za alama zetu za biashara (pamoja, “Deriv IP”). Tunakupatia leseni isiyoweza kukabidhiwa, isiyoweza kuhamishwa, isiyoweza kugawiwa, na inayoweza kufutwa ya kutumia Deriv IP kwa madhumuni ya pekee ya kutangaza bidhaa za Deriv na/au uhusiano wako nasi kama Mshirika (Affiliate), kwa masharti kwamba:
5.3.1. Matumizi yako ya Deriv IP yawe sambamba na mwongozo wetu wa masoko na utangazaji wa Deriv, miongozo mingine yoyote ya masoko, na maelekezo yoyote ambayo tunaweza kukupatia mara kwa mara;
5.3.2. Unakubali kwamba sifa njema yoyote itakayotokana na matumizi yako ya Deriv IP itatunufaisha sisi, na iwapo tutaomba, utakamilisha mara moja hati yoyote inayothibitisha uhamishaji wa sifa hiyo njema kwetu;
5.3.3. Usifanye, wala usijaribu kufanya, kitendo chochote kinachoweza kudhoofisha, kuharibu, au kuathiri vibaya Deriv IP au sifa na heshima inayohusiana nasi au Deriv IP, au kitendo chochote kinachoweza kubatilisha au kuhatarisha usajili wa alama yoyote ya biashara iliyo ndani ya Deriv IP;
5.3.4. Hutafanya maombi ya usajili, wala hupaswi kupata usajili wa alama yoyote ya biashara au huduma, jina la biashara, au jina la tovuti katika nchi yoyote duniani ambalo linafanana au linajumuisha, au ambalo kwa maoni yetu ya msingi linafanana kwa njia ya kupotosha na Deriv IP, wala huruhusiwi kuruhusu, kushawishi, au kusaidia mtu mwingine kufanya hivyo;
5.3.5. Iwapo utagundua ukiukwaji wowote wa kweli, unaoshukiwa, au unaotishia Deriv IP, au madai kwamba Deriv IP yoyote inakiuka haki za mtu mwingine, utatufahamisha mara moja;
5.3.6. Iwapo unataka kutengeneza bidhaa zozote za kimwili au bidhaa za biashara zenye Deriv IP, lazima upate idhini yetu ya maandishi ya awali kwa kutuma barua pepe kwenda [email protected] na nakala kwa msimamizi wako wa akaunti ya mshirika (affiliate); na
5.3.7. Haupaswi kubadilisha au kufanya mabadiliko yoyote kwenye sehemu yoyote ya nyenzo zetu za masoko bila idhini ya maandishi kutoka kwetu.
5.4. Haupaswi kulenga, kupitia shughuli zozote za masoko, matangazo, au promosheni unazofanya, wateja wote walio chini ya umri wa kisheria unaohitajika kufanya biashara katika nchi wanayoishi.
5.5. Haupaswi kuendeleza na/au kutekeleza shughuli za masoko, matangazo, na promosheni unazofanya ambazo zinakiuka sheria, kanuni, taratibu, au kanuni za maadili zinazohusiana na masoko, matangazo, na shughuli za promosheni zinazohusika (ikiwa ni pamoja na chini ya mamlaka ya chombo chochote cha udhibiti, wakala wa serikali, au mamlaka ya utekelezaji wa sheria) katika maeneo yoyote unayofanyia kazi au kulenga biashara.
5.6. Haupaswi kuiga kikoa cha tovuti zetu au kununua, kuomba, au kusajili maneno yoyote ya msingi, maneno ya utafutaji, au vitambulisho vingine kwa matumizi katika injini yoyote ya utafutaji, portal, huduma ya matangazo ya kudhaminiwa, au huduma nyingine yoyote ya utafutaji au uelekezaji, katika kila hali ambayo ni sawa au inafanana na alama zetu za biashara au majina ya kibiashara yanayojumuisha neno "Deriv" au mabadiliko yoyote ya neno hilo.
5.7. Matangazo na kampeni zako hazipaswi kuelekeza trafiki moja kwa moja kwenye tovuti zetu na hayapaswi kujumuisha URL yoyote yenye neno “Deriv” au toleo lolote la neno hilo.
5.8. Hatuvumilii usambazaji wa ujumbe wowote usiomuhimu au usiotakiwa unaotumwa kupitia mtandao kwa idadi kubwa ya watumiaji kwa madhumuni ya kutangaza, kuhadaa (phishing), au kusambaza programu hasidi (“Spam”). Iwapo utatuma, utazalisha, utasambaza, au kueneza kwa njia yoyote ile aina yoyote ya Spam, akaunti yako inaweza kuwekwa chini ya uchunguzi, na fedha zote unazodai zinaweza kuzuiwa hadi uchunguzi wa akaunti yako utakapokamilika. Kwa kuwa tunawajibika kulipa faini kwa sababu ya Spam na huenda tukapata madhara kwa sifa yetu mbele ya wateja, tunaweza kukata fidia yoyote, gharama, au matumizi yanayohusiana kutoka kwenye akaunti yako (“Gharama za Spam”). Iwapo hili litatokea, tutakadiria kiasi cha Gharama za Spam kwa nia njema na kwa njia ya haki, ingawa kumbuka kwamba uamuzi wetu utakuwa wa mwisho. Kwa kujisajili kama Mbia wa Biashara, unakubali kuwa hii ni fidia ya haki na inayofaa kwetu kwa sababu ya kutuma Spam.
5.9. Iwapo salio la akaunti yako halitoshi kufidia Gharama zozote za Spam, tuna haki ya kuchunguza njia mbadala za kupata malipo. Kwa mfano, ikiwa shughuli zako kama Mshirika (Affiliate) zimesababisha kufunguliwa kwa akaunti za ununuzi, huenda tusikulipe gawio kwa akaunti hizo hadi kiasi unachodaiwa kwa ajili ya Gharama za Spam kitakapolipwa kikamilifu.
5.10. Unakubali kufichuliwa kwa utambulisho wako kwenye tovuti zetu au kwenye njia yoyote ya mawasiliano ya umma tunayoisimamia.
5.11. Iwapo utapewa bidhaa yoyote yenye chapa ya Deriv kwa ajili ya kuwasambazia wateja wako au wateja watarajiwa, unakubali kutotoza ada yoyote kwa bidhaa hiyo.
5.12. Hupaswi kushiriki katika shughuli zozote zinazozidi uvumilivu wa mifumo yetu ya ndani au zinazotoka nje ya mipaka ya shughuli za kawaida za biashara, kama inavyobainishwa kwa hiari yetu pekee. Hii inajumuisha kusambaza upya Deriv feed, kutumia rasilimali zetu za mfumo kupita kiasi, au kujaribu kwa nia mbaya kuvuruga utendakazi wa kawaida wa mifumo yetu kupitia maombi au trafiki kupita kiasi. Iwapo utakiuka kifungu hiki, tuna haki ya kuchukua hatua yoyote tunayoona kuwa ni muhimu na kurejesha gharama zozote zilizotokea kutokana na ukiukaji huo.
6. Makongamano na hafla
6.1. Sehemu hii inajumuisha vigezo na masharti yanayokuhusu endapo utahudhuria au unapanga kuhudhuria makongamano au hafla yoyote katika nafasi yako kama Mshirika (Affiliate) na/au Broker Mwakilishi (kila “Hafla”).
6.1.1. Tutabainisha na kukwambia mahali Hafla inapofanyika. Tuna haki ya kufuta mwaliko au kubadilisha tarehe na/au mahali pa Hafla.
6.1.2. Ushiriki katika Hafla ni kwa Washirika (Affiliates) na Brokers Wawakilishi walioalikwa kwa maandishi na (iwapo inahitajika) wageni wowote walioruhusiwa katika mwaliko huo. Wageni lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi.
6.1.3. Huwezi kuhamisha mwaliko wako kwa mtu mwingine, na huwezi kuongeza muda wa ushiriki wako zaidi ya tarehe zilizotajwa katika mwaliko wako.
6.1.4. Unakubali kutupatia uthibitisho wa kitambulisho chako pamoja na cha mgeni/wageni wako, pamoja na hati nyingine zozote zilizotajwa kwenye barua pepe ya mwaliko wako. Tuna haki ya kufuta mwaliko wako na/au kuwazuia mgeni/wageni wako kushiriki katika Hafla ikiwa hatutapokea hati zilizoombwa.
6.1.5. Tuna haki ya kuchagua uwanja wa ndege unaofaa wa kuwasili/kuondoka kwa ajili ya Hafla, ambao utakuwa sawa kwako na kwa mgeni/wageni wako.
6.1.6. Tuna haki ya kugawa vyumba na kubadilisha ugawaji wa vyumba au utaokaanao kwenye chumba kulingana na upatikanaji na kipaumbele.
6.1.7. Iwapo wewe na/au mgeni/wageni wako mtakosa ndege ya kuunganisha, kufika kwa kuchelewa kwenye Hafla, au kutofika kabisa kwenye Hafla, gharama zozote zitakazojitokeza kutokana na kughairi kwa dharura zitakuwa juu yako. Baada ya uthibitisho wako wa maandishi wa kupewa tiketi ya ndege, gharama za mabadiliko au kughairiwa kwa safari ambazo hazijafanywa na sisi zitakuwa juu yako endapo marejesho ya fedha hayatawezekana.
6.1.8. Iwapo wewe na/au mgeni/wageni wako hamtaweza kuhudhuria Hafla, unapaswa kumjulisha mwanachama wa timu yako ya mshirika/msimamizi wa akaunti kupitia barua pepe au WhatsApp si chini ya wiki mbili (2) kabla ya Hafla. Baada ya tarehe ya mwisho iliyowekwa, ada yoyote ya kughairi itatozwa kwako.
6.1.9. Mwaliko wa Hafla unagharamia tu matumizi ya kukaa kwako (chakula na hoteli), tiketi ya ndege, na usafiri kutoka uwanja wa ndege hadi hotelini na kutoka hotelini hadi uwanja wa ndege kwa ajili yako na mgeni/wageni wako (panapohusika). Vipimo vyovyote vya kitabibu au chanjo ambazo huenda zikahitajika kwa ajili ya safari havijajumuishwa. Ni jukumu lako kukagua huduma zilizojumuishwa katika kifurushi cha hoteli kilichojumuishwa kwenye mwaliko wako. Utawajibika kulipia gharama zozote za ziada zilizotozwa kwenye chumba chako wakati wa kuondoka hotelini.
6.1.10. Tunaweza kuandalia bima ya safari kwa ajili yako na/au mgeni wako. Iwapo tutafanya hivyo, wewe na mgeni/wageni wako mtakuwa mmehakikishwa na bima ya usafiri tunayoidhamini, kulingana na masharti na vigezo vya sera hiyo. Iwapo wewe au mgeni wako mtaamua kuendelea kukaa baada ya kipindi cha Hafla, ni jukumu lenu kupanga bima ya usafiri kwa kipindi cha nyongeza. Tunaweza kupendekeza upate bima ya kusafiri kwa kujitegemea ili kuhakikisha unalindwa katika hali zote.
6.1.11. Kwa kushiriki katika Hafla, unatupa ruhusa ya kupiga na kuchapisha picha na video ambazo unaweza kuwemo kwa madhumuni ya masoko na matangazo. Ikiwa hutaki tutumie picha au video zozote zinazokuonyesha, tafadhali tutumie barua pepe kwa anwani [email protected] ili kuwasilisha ombi lako kwa maandishi.
6.1.12. Unatakiwa kupata ruhusa ya wazi kutoka kwetu kabla ya kutumia picha na/au video zozote zilizopigwa wakati wa Hafla katika maudhui yako.
6.1.13. Wewe na mgeni/wageni wako mnapaswa kufuata miongozo ya hoteli pamoja na sheria, desturi, na taratibu za eneo husika. Tuna haki, bila kuwajibika kisheria, kukukatalia kuingia au kukuondoa kwenye Hafla ikiwa tutakuona kuwa unahatarisha usalama au kuleta usumbufu kwa uendeshaji mzuri wa Hafla.
6.1.14. Hatutawajibika kutekeleza majukumu yetu yoyote yanayohusiana na Hafla iwapo hatutaweza kufanya hivyo kutokana na hali zisizotarajiwa au hali zilizo nje ya uwezo wetu wa kudhibiti. Hatutawajibika kukulipa fidia wewe na/au mgeni wako katika hali kama hii.
6.1.15. Unakubali kutulinda na kutuondolea hatia kutokana na madai yoyote dhidi yetu yatakayowasilishwa na wewe na/au mgeni/wageni wako kwa sababu yoyote ya jeraha dogo, jeraha kubwa, au ugonjwa (kama COVID-19), ambayo ni hatari asili zinazohusiana na shughuli za mwili na wakati wa kutekeleza au kushiriki katika shughuli yoyote kama hiyo.
6.1.16. Unakubali kutulinda na kutuondolea hatia kutokana na madai yoyote dhidi yetu yanayotolewa na wahusika wengine (kama vile mkeo, mumeo, au wategemezi wako) ikiwa, wakati wa Hafla, mali zako au za mgeni wako zitaharibiwa, au wewe au mgeni wako mtapotea, kujeruhiwa, au kupoteza maisha.
6.1.17. Unakubali kutulinda sisi na wawakilishi wetu na kutuondolea hatia dhidi ya gharama zote, madai, uharibifu, majukumu, na matumizi (pamoja na ada zozote za kitaalamu) ambazo tunaweza kuzipata kutokana na ukiukaji wa Masharti haya na wewe au mgeni/wageni wako.
6.2. Kanuni za maadili
6.2.1. Washiriki wote wanapaswa kuonyesha tabia inayofaa, kudumisha mwenendo wa kitaaluma, na kuchangia katika mazingira ya heshima kwa wafanyakazi na watu wengine wanaohusika katika Hafla, mikutano, au shughuli mbalimbali. Kama kampuni, tunashiriki maadili kama usawa wa utoaji haki, heshima, utu, na kupinga aina yoyote ya tabia inayojumuisha unyanyasaji wa maneno au wa kimwili.
6.2.2. Tabia isiyofaa
6.2.2.1. Orodha ifuatayo ya tabia inachukuliwa kuwa haifai kwa kipindi chote cha Hafla, mkutano, au shughuli, iwe ya ana kwa ana au ya mtandaoni:
6.2.2.1.1. Matumizi ya aina yoyote ya maneno ya kukashifu, kudhalilisha, au kutisha
6.2.2.1.2. Aina zote za unyanyasaji au shinikizo la kingono kwa njia ya kimwili au ya maneno, ikiwa ni pamoja na vitendo vya kudokeza mambo ya kingono au ya faragha, kugusana kimakusudi, matumizi ya lugha chafu na isiyofaa kwa njia yoyote ile (kama vile kwa kuzungumza, kuandika, au kwa mawasiliano ya kidigitali, n. k.)
6.2.2.1.3. Matamshi yenye maudhui ya ubaguzi wa kijinsia au chuki dhidi ya watu wa mataifa au asili tofauti, ambayo yanaweza kusababisha mazingira ya kutojisikia vizuri, ya matusi, au ya ubaguzi
6.2.2.1.4. Vitendo vya moja kwa moja au visivyo vya moja kwa moja vya ukatili ambavyo si vya kingono, ikiwa ni pamoja na tabia, vitendo, au maoni yoyote ya kibaguzi, kutisha, kukashifu, au vitisho
6.2.2.1.5. Kitendo chochote cha vurugu, iwe ni ya kimwili au ya maneno, kupitia njia zote za mawasiliano zilizopo (ana kwa ana, kupitia mitandao ya kijamii, ujumbe binafsi, n. k.)
Uvunjaji wowote wa Kifungu hiki 6.2.2 utatathminiwa kwa kuzingatia mazingira ya kila tukio, na tunaweza kuchukua hatua zinazofaa kwa hiari yetu, ikiwa ni pamoja na hatua kama kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe bila taarifa.
6.2.3. Matokeo ya tabia zisizofaa
6.2.3.1. Kulingana na uzito wa kitendo, ambao utaamuliwa kwa mujibu wa vigezo vyetu pekee na/au vigezo vya mratibu mwingine yeyote wa Hafla, mkutano, au shughuli, hatua zifuatazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya mtu aliyekemewa:
6.2.3.1.1. Uzito mdogo
6.2.3.1.1.1. Mara ya kwanza: Kikao kinafanyika, na onyo linatolewa kwa mshambuliaji.
6.2.3.1.1.2. Mara ya pili: Tuna haki ya kutomjumuisha mshambuliaji katika hafla zijazo.
6.2.3.1.1.3. Kurudiwa kwa kosa au kosa kubwa la kwanza: Iwapo kutatokea makosa ya mara kwa mara kutoka kwa mhudhuriaji, au kama kosa la kwanza limehatarisha usalama, heshima, na utu wa aliyeshambuliwa, tutazingatia kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara na wewe. Tumechagua kutojihusisha na watu ambao hawazingatii maadili yetu. Uamuzi utawasilishwa kwa maneno na kwa maandishi kwa wahusika wote.
6.2.3.1.2. Uzito mkubwa
6.2.3.1.2.1. Manufaa na huduma zote zinazotolewa na sisi zinafutwa. Mshambuliaji atatozwa gharama za malazi pamoja na gharama nyingine zote alizosababisha.
6.2.3.1.2.2. Mhanga ana haki ya kuripoti tukio hilo kwa mamlaka za eneo husika.
7. Uwakilishi na dhamana
7.1. Unawakilisha, unadhamini, na unakubali kwamba:
7.1.1. Taarifa zote ulizotupatia wakati wa mchakato wa kujisajili ni za kweli, sahihi, na hazipotoshi;
7.1.2. Utakuwa ukifanya kila jambo kwa nia njema katika mahusiano yako nasi;
7.1.3. Umepata na utaendelea kuwa na leseni na idhini zote muhimu za kuendesha shughuli zako kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zinazotumika (ikiwemo zile chini ya mamlaka ya chombo chochote cha udhibiti, wakala wa serikali, au mamlaka ya utekelezaji wa sheria) katika maeneo unakoendesha au kulenga biashara;
7.1.4. Hauna taarifa yoyote inayojulikana ambayo inaweza, au kwa msingi wa hoja za msingi inatarajiwa, kukuzuia au kuathiri utendaji wako wa majukumu yoyote chini ya Masharti ya Biashara kwa njia na wakati uliokusudiwa na Masharti haya ya Biashara;
7.1.5. Tovuti yako au nyenzo zako za matangazo hazitapaswa kuwa na maudhui yoyote ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa ya kashfa, ponografia, kinyume cha sheria, hatarishi, ya vitisho, matusi, ya unyanyasaji (ikiwemo ya kibaguzi au ya kikabila), au maudhui mengine yasiyofaa, ya kibaguzi, ya vurugu, ya kisiasa au yenye utata, au yanayokiuka haki miliki za mtu mwingine yeyote (kwa mfano, hakimiliki, hati miliki, au alama ya biashara) au haki nyingine za mali ya mtu au shirika lolote;
7.1.6. Hauna rekodi ya kihalifu inayohusiana na rushwa na ufisadi, mauaji, ugaidi, usafirishaji haramu, uhalifu wa kifedha, au kosa lolote jingine ambalo linaweza kukufanya usifae kuingia au kudumisha uhusiano wa kibiashara nasi;
7.1.7. Utafuata Sera Yetu ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi katika kipindi chote cha uhusiano wa kibiashara;
7.1.8. Hujawahi na hutatijihusisha na shughuli yoyote ambayo, kupitia uhusiano wako nasi, inaweza kuharibu sifa ya Deriv; na
7.1.9. Hutatumia wala kumruhusu mtu mwingine yeyote kutumia bidhaa na huduma zetu kwa madhumuni ya utakatishaji wa fedha, ufadhili wa ugaidi, au shughuli nyingine zozote za kihalifu.
7.2. Tunatoa tovuti yetu kwa msingi wa “ilivyo” na “inavyopatikana” bila dhamana yoyote kwamba itakuwa haina hitilafu, kwamba hitilafu zozote zitasahihishwa, au kwamba tovuti yetu haina mwingilio wowote kutoka kwa watu wengine kama vile wahalifu wa mtandaoni au vipengele vingine hatari vinavyotokea nje ya uwezo wetu wa kudhibiti.
7.3. Hatutoi ahadi yoyote kwamba tovuti yetu au bidhaa zetu zitapatikana bila usumbufu wowote au kwamba huduma itatolewa bila makosa. Hatutawajibika kwa madhara yoyote yatokanayo na makosa au usumbufu wa aina hiyo.
8. Fidia na dhima
8.1. Utatulipa fidia na kutulinda dhidi ya hasara, madai, malalamiko, uharibifu, gharama, matumizi, na wajibu wowote (ikiwemo hasara za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja, upotevu wa faida, na gharama halali za kisheria, iwapo zitahusika) ambazo tunaweza kupata au kuelemewa nazo, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kutokana na matendo yako au ya washirika wako wowote, mawakala, na/au wafanyakazi wako:
8.1.1. Uvunjaji, kutotekeleza, au kutokuzingatia wajibu au dhamana yoyote uliyo nayo chini ya Masharti ya Biashara; au
8.1.2. Ulaghai, kuacha kutekeleza jambo, uzembe, utovu wa nidhamu, au upotoshaji wa taarifa.
8.2. Iwapo tutagundua kuwa unakiuka masharti yoyote yaliyoainishwa katika Masharti ya Biashara, pamoja na haki au suluhisho lolote tulilo nalo chini ya Masharti ya Biashara au sheria yoyote inayotumika, tutakuwa na haki ya kusitisha mara moja uhusiano wa kibiashara kati yetu na wewe na kufuta haki zako zote kama Mbia wetu wa Biashara. Unakiri na unakubali kwa dhati kuachana kabisa na haki na madai yoyote dhidi yetu, na unatuachilia huru na kutulinda sisi, kampuni zetu washirika, wakurugenzi wetu, maafisa, wanahisa, wafanyakazi, au tovuti zetu dhidi ya uwajibikaji wowote endapo tutachukua hatua yoyote dhidi yako.
8.3. Hakuna chochote katika Masharti haya ya Biashara kitakachopunguza au kuondoa uwajibikaji wetu kwa jambo lolote ambalo haliwezi kupunguzwa au kuondolewa chini ya sheria husika.
8.4. Unatekeleza huduma zako na majukumu mengine yaliyoainishwa katika Masharti haya ya Biashara kwa gharama na hatari zako mwenyewe. Kulingana na Kifungu cha 8.3, hatutawajibika kwako kwa mkataba, kwa madhara (tort), au vinginevyo (ikiwemo uwajibikaji kwa uzembe) kwa hasara au uharibifu wowote, wa aina yoyote au uliosababishwa kwa njia yoyote, unaotokea moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusiana na Masharti haya ya Biashara au uhusiano wa kibiashara, ikiwa ni pamoja na (a) hasara yoyote ya biashara, mapato, faida au akiba iliyotarajiwa; (b) matumizi yoyote yaliyopotea bure, rushwa au uharibifu wa data; (c) kupoteza sifa njema au jina zuri la biashara; au (d) hasara yoyote ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja.
8.5. Ni wewe pekee utakayewajibika kwa ukuzaji, uendeshaji, na matengenezo ya tovuti yako (au tovuti zako) na kwa maudhui yote yanayoonekana kwenye tovuti yako (au tovuti zako) au unayochapisha kwenye tovuti nyingine. Utatulipa fidia na kutulinda dhidi ya hasara, madai, malalamiko, uharibifu, gharama, matumizi, na wajibu wote (ikiwemo hasara zisizo za moja kwa moja, upotevu wa faida, na gharama halali za kisheria iwapo zitahusika) ambazo tunaweza kupata au kuelemewa nazo, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kuhusiana na ukuzaji, uendeshaji, matengenezo, na maudhui ya tovuti yako (au tovuti zako), au maudhui uliyochapisha kwenye tovuti nyingine.
8.6. Kulingana na Kifungu cha 8.3, hatutawajibika kwa mteja yeyote kutokana na ulaghai wako, kutokutekeleza jambo, uzembe, mwenendo mbaya, upotoshaji wa taarifa, au makusudi ya kutotimiza wajibu, au ikiwa utakiuka Masharti ya Biashara kwa njia nyingine yoyote.
8.7. Kulingana na Kifungu cha 8.3, hatutawajibika kwa njia yoyote ile kwa ushauri wowote wa kifedha au uwekezaji au huduma nyingine yoyote utakayotoa kwa mteja yeyote kinyume na Masharti ya Biashara.
9. Usiri
9.1. Unakubali kwamba, katika kipindi cha uhusiano wetu wa kibiashara kulingana na Masharti ya Biashara, unaweza kupata taarifa zinazotuhusu sisi, kampuni zetu mama, kampuni tanzu, washirika, wateja, au watu wengine, kwa mfano, zinazohusiana na utambulisho wa mteja, hali ya kifedha, shughuli za biashara au utendaji wa miamala, pamoja na mipango yetu ya biashara, viwango vya bei, mawazo, dhana, miundo, mapendekezo, maendeleo, mipangilio, programu, mbinu, methodolojia, maarifa ya kiufundi, zana na vifaa, au taarifa nyingine yoyote ambayo kwa mantiki inaweza kuchukuliwa kuwa ya siri (kwa pamoja, “Taarifa za Siri”).
9.2. Hutapaswa kufichua Taarifa za Siri kwa mtu mwingine yeyote. Wajibu huu utaendelea kutumika hata baada ya kusitishwa kwa uhusiano wa kibiashara.
9.3. Hutaruhusiwa kuzalisha nakala zozote za Taarifa za Siri au maudhui yoyote yanayotokana na Taarifa za Siri kwa matumizi binafsi, usambazaji, au kwa njia nyingine yoyote bila ombi letu au idhini yetu ya maandishi.
9.4. Unatakiwa kuhakikisha kwamba washirika wako wote, wafanyakazi, na mawakala wanazingatia masharti yaliyoainishwa katika Kifungu hiki cha 9.
9.5. Iwapo uhusiano wa kibiashara kati yako na sisi utasitishwa, utarejesha kwetu mara moja nakala zote za Taarifa za Siri na nyaraka zote zilizo mikononi mwako zinazohusiana na biashara yetu.
10. Force majeure (Hali ya dharura ambayo haijatarajiwa)
10.1. Hatutawajibika kwa kutotekeleza au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yoyote kwa kiwango ambacho tukio lililo nje ya uwezo wetu wa kawaida wa kudhibiti limesababisha ucheleweshaji au kushindwa huko.
10.2. Iwapo utashindwa kutekeleza majukumu yako chini ya Masharti ya Biashara kutokana na tukio lililo nje ya uwezo wako wa kawaida wa kudhibiti, ni lazima utujulishe kwa maandishi ndani ya siku tatu (3) baada ya kutokea kwa tukio hilo.
11. Usitishaji
11.1. Tunaweza kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe wakati wowote kwa kukupa taarifa ya maandishi angalau siku saba (7) kabla.
11.2. Unaweza kusitisha uhusiano wako wa kibiashara nasi wakati wowote kwa kutupatia taarifa ya maandishi angalau siku saba (7) kabla.
11.3. Tunaweza kusitisha uhusiano wetu wa kibiashara nawe mara moja bila kutoa taarifa ya awali:
11.3.1. Iwapo utashindwa kulipa madeni yako yanapostahili kulipwa, au ukafilisika au kutokuwa na uwezo wa kifedha, kama inavyofafanuliwa chini ya sheria yoyote inayohusika ya kufilisika au ya ufilisi;
11.3.2. Iwapo mpokeaji, mkaguzi au msimamizi atateuliwa kusimamia biashara yako yote au sehemu yoyote ya biashara yako au mali zako, au ukafutwa kwenye daftari la kampuni katika mamlaka ambako umeandikishwa, au agizo likatolewa au azimio kupitishwa la kufunga kampuni;
11.3.3. Iwapo utakiuka Masharti haya ya Biashara kwa kiasi kikubwa;
11.3.4. Iwapo taarifa ulizotoa wakati wa mchakato wa usajili zitabainika kuwa za uwongo au si sahihi;
11.3.5. Iwapo shauri lolote la kisheria, hatua, au mchakato mwingine wa kisheria au kiutawala utaanzishwa dhidi yako kuhusiana na Masharti ya Biashara, au ikiwa sehemu au mali zako zote, shughuli zako, au rasilimali zako, iwe za kushikika au zisizoshikika, zitazuiliwa au kuwekewa vizuizi kutokana na mchakato huo;
11.3.6. Iwapo tabia yako itahusisha uzembe, udanganyifu, utovu wa nidhamu, upotoshaji, au makosa ya makusudi;
11.3.7. Iwapo utafanya ulaghai au kutumia vibaya uhusiano wa kibiashara kwa njia yoyote ile (na endapo ulaghai au matumizi mabaya yatagundulika, hatutawajibika kwako kwa gawio lolote kutokana na mauzo ya ulaghai au mauzo yoyote yanayotokana na matumizi mabaya);
11.3.8. Iwapo tunaamini kwamba unakiuka au umekiuka sheria, kanuni, taratibu, au misingi ya maadili (ikiwa ni pamoja na ile inayohusiana na masoko, matangazo, na shughuli za promosheni) ambazo zinaweza husika au kutumika katika mamlaka unakofanyia biashara au unakolenga biashara;
11.3.9. Iwapo tunaamini kwamba unakiuka au umekiuka sheria yoyote, kanuni, taratibu, au kanuni za maadili (ikiwemo ile inayohusu masoko, matangazo, na shughuli za promosheni) ambazo zinaweza husika au kutumika katika mamlaka unayofanyia au unayolenga kufanya biashara;
11.3.10. Iwapo uwezo wako wa kutekeleza majukumu na wajibu wowote chini ya Masharti ya Biashara utapungua kwa kiasi kikubwa;
11.3.11. Iwapo tutagundua kwamba umejihusisha na makubaliano au mienendo ya kupinga ushindani, ikiwa ni pamoja na kupanga bei, kuweka mipaka ya utoaji wa huduma, udanganyifu wa bei, na/au kugawana soko;
11.3.12. Ikiwa tutabaini kwamba umejihusisha na shughuli yoyote ambayo sisi, kwa uamuzi wetu pekee, tunachukulia kuwa inaharibu sifa ya Deriv (tuna haki ya kuzuia, kama fidia, kiasi chochote tunachoona kinastahili kulipwa kuhusiana na madhara ya kisifa ambayo Deriv imepata); au
11.3.13. Kama ilivyoainishwa katika Vifungu 3.5.2, 4.2, 4.5, 4.6, na 8.2 au kama ilivyoelezwa katika Masharti ya Ziada yanayokuhusu wewe.
11.4. Kusitishwa kwa uhusiano wa kibiashara kati yako na sisi hakutagusa haki zetu, ambazo zinaweza kuwa zimeshaanza au zimekusanywa au kabla ya tarehe ya kutamatika kwa uhusiano.
11.5. Unakubali kwamba baada ya kusitishwa, huna madai yoyote dhidi yetu na hustahili fidia yoyote au madai yatokanayo na kusitishwa huko.
11.6. Baada ya kusitishwa kwa Masharti haya ya Biashara, utalazimika:
11.6.1. Haraka unapaswa kusitisha kutaja Deriv na kutumia IP ya Deriv (iwe kwa nakala ngumu au kielektroniki kwenye tovuti yoyote);
11.6.2. Kurejesha haraka nyenzo zote zinazohusisha Deriv IP kwetu kwa gharama yako; na
11.6.3. Kuondoa mara moja alama zote za biashara za Deriv, ikiwemo logo, chapa, na marejeleo mengine ya Deriv, kutoka kwenye tovuti yako na/au nyenzo zako za masoko.
11.7. Kusitishwa hakutabatilisha uvunjaji wowote wa Masharti ya Biashara na hakutakuondoa kwenye uwajibikaji wowote kwa uvunjaji wa wajibu wako chini ya Masharti ya Biashara.
12. Mawasiliano na malalamiko
12.1. Chagua anwani ya barua pepe ya kututumia mawasiliano yako kwa ujumla kulingana na nafasi yako: Washirika na Broker Wawakilishi wanapaswa kutumia [email protected] kwa maswali ya jumla. Wakala wa Malipo wanapaswa kuwasiliana na [email protected], na Watumiaji wa API wanapaswa kuwasiliana na [email protected].
12.2. Kwa taarifa au malalamiko yanayohusu Masharti haya ya Biashara, tafadhali yatume kwa maandishi kwa [email protected] na pia anwani ya barua pepe inayolingana na nafasi yako, iliyoelezwa katika kifungu kilichotangulia.
12.3. Taarifa yoyote au mawasiliano yanayohitajika au yanayoruhusiwa kutolewa chini ya Masharti haya ya Biashara yatakuwa kwa maandishi na yatachukuliwa kuwasilishwa, kutolewa, na kupokelewa ipasavyo wakati yamepelekwa kwenye anwani ya barua pepe ya mpokeaji. Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “Siku za Biashara” zinarejelea siku za kibiashara katika mamlaka ya upande wako wa mkataba wa Masharti haya ya Biashara (kama ilivyowekwa katika Vifungu 1.3 na 1.4). Taarifa yoyote itakayotumwa kwa barua pepe itahesabiwa kuwa imepokelewa siku ya biashara inayofuata baada ya siku ambayo ilitumwa. Iwapo siku ambayo taarifa inachukuliwa kupokelewa si Siku ya Kibiashara, basi taarifa hiyo inachukuliwa kupokelewa siku ya biashara inayofuata.
12.4. Iwapo utatuma malalamiko kwetu, tutakubali kupokea malalamiko yako kupitia barua pepe, tutachunguza malalamiko yako, na kutuma jibu la mwisho ndani ya siku kumi na tano (15) tangu tarehe ambayo malalamiko yamepokelewa.
12.5. Ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unaweza kupokea barua pepe zote tunazotuma kwako.
13. Sheria zinazoongoza na mamlaka
13.1. Masharti haya ya Biashara na migogoro yoyote inayotokana na, kuhusiana na, au inayohusiana na tafsiri ya Masharti haya ya Biashara (pamoja na migogoro isiyo ya mkataba) itatawaliwa na sheria za mamlaka ya upande wako wa mkataba, kama ifuatavyo:
13.1.1. Deriv (FX) Ltd: Labuan, Territory of Malaysia;
13.1.2. Deriv (BVI) Ltd: Visiwa vya Virgin vya Uingereza;
13.1.3. Deriv (V) Ltd: Vanuatu; au
13.1.4. Deriv (SVG) LLC: Saint Vincent na Grenadines.
13.2. Unakubali kuwa chini ya mamlaka ya mahakama katika mamlaka ya upande wako wa mkataba (kama ilivyowekwa katika Kifungu cha 13.1) na kuwasilisha madai yoyote unayoweza kuwa nayo mbele yao. Mahakama hizi zitakuwa na mamlaka pekee ya kusuluhisha migogoro yoyote inayoweza kutokea kati yako na sisi.
14. Mambo Mengine
14.1. Masharti haya ya Biashara yanaunda mkataba kamili kati yako na sisi na yanabatilisha makubaliano yote ya awali, ahadi, hakikisho, na uwakilishi wowote (wa maandishi au ya mdomo) yanayohusiana na mada yake.
14.2. Unatambua kwamba wewe ni huru na hatuhusiani moja kwa moja, na kwamba kukubali Masharti ya Biashara kwa namna yoyote hakutaunda ushirikiano, mradi wa pamoja, uwakala, franchise, uwakilishi wa mauzo, uhusiano wa kifedha, au uhusiano wa ajira kati yako na sisi. Hutakuwa na mamlaka ya kufanya au kukubali ofa au uwakilishi wowote kwa niaba yetu. Hutatoa tamko lolote, iwe kwenye tovuti yako au vinginevyo, ambalo kwa hali ya kawaida lingepingana na chochote kilichoainishwa katika Kifungu hiki 14.2.
14.3. Unaelewa kwamba uhusiano kati yako na sisi si wa kipekee na kwamba tunaweza kuingia katika uhusiano sawa na mtu mwingine yeyote bila kikwazo.
14.4. Tunaweza kuhamisha baadhi au haki zetu zote chini ya Masharti ya Biashara kwa upande mwingine.
14.5. Huwezi kutoa haki zako zote au baadhi chini ya Masharti ya Biashara kwa wahusika wengine bila idhini yetu ya maandishi ya awali.
14.6. Iwapo kipengele chochote cha Masharti haya ya Biashara kitapatikana kuwa batili au hakiwezi kutekelezwa na mahakama yoyote au chombo cha kiutawala chenye mamlaka husika, ubatili au kutotekelezeka huko hakutaathiri vifungu vingine vya Masharti haya ya Biashara, ambavyo vitaendelea kuwa na nguvu na kutumika kikamilifu.
14.7. Iwapo tutashindwa kusisitiza kwamba utekeleze majukumu yako yoyote chini ya Masharti haya ya Biashara, ikiwa hatutatekeleza haki zetu dhidi yako, au tukichelewa kufanya hivyo, haitamaanisha kwamba tumekataa haki zetu dhidi yako wala haitamaanisha kwamba huna wajibu wa kutekeleza majukumu hayo. Iwapo tutakubali msamaha wa makosa yako, tutafanya hivyo tu kwa maandishi, na hilo halitamaanisha kwamba tutakubali moja kwa moja makosa yoyote ya baadae utakayoyafanya.
14.8. Iwapo Masharti haya ya Biashara yatatafsiriwa katika lugha nyingine yoyote, na kutakuwa na tofauti kati ya maandishi ya Kiingereza na maandishi yaliyotafsiriwa, maandishi ya Kiingereza ndiyo yatakayozingatiwa.
1. Utangulizi
Mwongozo huu umebuniwa ili kusaidia kukuza Deriv kwa ufanisi na kwa maadili. Kwa kufuata sheria hizi, unaweza kujenga imani na wateja wako na kuwakilisha maadili ya Deriv. Tafadhali soma mwongozo huu kwa uangalifu. Kama hutatii sheria hizi, tunaweza kuhitaji kumaliza ushirikiano wetu. Ikiwa una maswali au unahitaji msaada, tafadhali wasiliana na Meneja wako wa Akaunti.
2. Miongozo ya uwekaji chapa na nembo

Daima onyesha kifungu “Powered by” juu au mbele ya nembo ya Deriv kwenye tovuti yako na katika programu zozote za simu unazounda.

Eleza wazi uhusiano wako na Deriv. Tumia misemo kama “ikiwa ni ushirikiano na Deriv” na “kwa kushirikiana na Deriv” au jitambulisha kama Deriv Affiliate.

Hauruhusiwi kuanzisha makundi au vituo ukitumia jina na nembo ya Deriv. Katika tovuti yako na majukwaa, huwezi:
- Kopisha blok za maudhui kutoka kwenye tovuti ya Deriv.
- Kutaja kanuni na maelezo ya wasimamizi wa Deriv.
- Kutumia maelezo ya wafanyakazi wa Deriv au picha kutoka kwenye tovuti ya Deriv.
3. Kuunda uwepo wako mtandaoni

Hifadhi mtindo wako binafsi. Epuka kutumia mpangilio wa rangi uleule na Deriv au majina yanayoonekana au kusikika kama Deriv.

Tengeneza uwepo wako wa kipekee mtandaoni kama mshirika wa Deriv. Hii inaweza kuwa kupitia tovuti yako binafsi au kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii. Kwa mfano, unaweza kutengeneza video zinazowasaidia wateja jinsi ya kuanza na Deriv au jinsi ya kufanya biashara.

Hakikisha majina yako ya mitandao ya kijamii na maeneo ya tovuti ni ya kipekee.
Usitumie au kujumuisha jina la kampuni Deriv katika jina lako la mtumiaji.
4. Miadala ya masoko na utangazaji.
Kabla ya kuendeleza Deriv kupitia matangazo yaliyo na malipo kwenye majukwaa kama Facebook au Google, wasilisha ombi kwa Meneja wa Akaunti yako au kupitia barua pepe kwa [email protected]. Jumuisha nakala ya tangazo, nyenzo za ubunifu (video/picha), maneno muhimu, na ukurasa wa mwisho unaolenga.
Usitoe zabuni kwa maneno yaliyotambulika katika kampeni za utafutaji zilizo na malipo (mfano, Google na Bing).
Maneno yasiyoruhusiwa: deriv, deriv app, deriv broker, dtrader, deriv trading, deriv live account, deriv trader, deriv virtual account, bot trading deriv, deriv.com, www.deriv.com, deriv.com login, deriv mt5 trading, automated trading deriv, deriv register, deriv cfd trading, automated trading deriv.
- Tumia nyenzo za masoko zilizopatikana kwenye dashibodi yako ya ushirika kuendeleza Deriv. Kama unataka kutengeneza nyenzo zako za masoko, hakikisha unatumia onyo sahihi la hatari.
- Usibadili, kuhariri, au kufanyia mabadiliko nyenzo za masoko zilizotolewa na Deriv. Hakuna kitu kinachopaswa kufunikwa, na aina ya herufi inapaswa kubaki ile ile.
5. Mbinu bora za promosheni.
- Panga kampeni zako za promosheni kwa uangalifu ili machapisho yako yasionekane kama spam.
- Epuka kutuma spam kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, makundi, barua pepe, au tovuti zako za ushirika.
- Endeleza Deriv vyema kwenye majukwaa halali ya mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook, Instagram, X, na Telegram.
- Usitumie matangazo ya aina ya pop-up au promosheni kwenye tovuti haramu kutangaza kiungo chako cha ushirika.
6. Mawasiliano na uwazi.

Eleza wazi huduma unazozikuza. Hakikisha inaonekana wazi kwamba unaunga mkono jukwaa la biashara na si kasino au mpango wa kupata pesa kwa haraka. Kwa mfano, huwezi kuwakilisha Deriv au bidhaa na huduma zake kama:
- Bidhaa ya kifahari.
- Jukwaa rahisi la kupata pesa.
- Fursa ya uwekezaji.
- Kitu chochote kinachohakikisha mapato au faida.

Jumuisha taarifa ifuatayo ya onyo la hatari mahali pa kuonekana (kama kichwa au chini ya tovuti yako, kwa fonti na ukubwa unaosomeka):
- “Deriv hutoa bidhaa tata, ikiwa ni pamoja na Options na CFDs, ambazo zina hatari kubwa. Biashara za CFDs zinahusisha mkopo, ambao unaweza kuongeza faida na hasara, na hivyo kusababisha kupoteza uwekezaji wako wote. Fanya biashara kwa pesa unazoweza kumudu kupoteza na usizumie mkopo kufanya biashara. Elewa hatari kabla ya kufanya biashara.”

Jumuisha taarifa ifuatayo ya onyo la hatari kwenye profaili zako za mitandao ya kijamii na kuiweka kama picha ya bango, kwenye wasifu, au chapisho lililotikiswa:
- “Deriv hutoa bidhaa tata (Options, CFDs) zenye hatari kubwa. Unaweza kupoteza uwekezaji wako wote. Fanya biashara kwa uwajibikaji na elewa hatari.”

Daima ongeza moja ya taarifa zifuatazo za onyo la hatari kwenye machapisho yako ya mitandao ya kijamii yanayohusiana na Deriv:
- “Biashara inambatana na hatari.”
- “Mtaji wako uko hatarini. Sio ushauri wa uwekezaji.”
7. Kuheshimu faragha
- Daima pata ruhusa kabla ya kupiga picha au kurekodi video zinazoonesha wafanyakazi wa Deriv katika hafla yoyote.
- Usishiriki picha, video, au simu zilizorekodiwa za hafla zinazohusisha wafanyakazi wa Deriv bila ruhusa wazi kwa maandishi.
8. Hitimisho
Kufuata miongozo hii kutakusaidia kujenga uwepo wa mtandaoni wenye sifa nzuri kama mshirika wa Deriv, kuimarisha imani kati ya wateja wako, na kuboresha juhudi zako za promosheni. Ushirikiano wetu unaimarishwa kwa heshima ya pamoja na kufuata viwango hivi. Kama una maswali au unahitaji msaada, usisite kuwasiliana na Meneja wako wa Akaunti.