Kuzuia ulaghai
Hadaa ni shambulio la mtandao ambapo wahalifu wanajaribu kuwaongoza wateja kufichua taarifa zao binafsi kama nenosiri zao au taarifa ya benki zao. Matapeli hujifanya kuwa kampuni halisi na huunda barua pepe bandia, akaunti za mitandao ya kijamii, na nambari za simu ili kukushawishi kuchukua hatua ambazo zinaweza kuhatarisha taarifa zako na usalama wako. Kubofya viunganishi (links) au faili hatarishi zilizo katika barua pepe za ulaghai kunaweza kupakua virusi kwenye kifaa chako na kufichua taarifa zako.
Kumbuka mambo 5 usiyopaswa kufanya:
1. Usibofye viunganishi (links) au kupakua faili papo hapo bila tahadhari.
2. Usitoe taarifa zako binafsi.
3. Usichukue hatua kwa haraka ikiwa unashinikizwa kufanya hivyo.
4. Usijibu barua pepe, simu na jumbe unazotilia mashaka.
5. Usiogope kuwasiliana na Msaada kwa Wateja ikiwa una mashaka au wasiwasi wowote.
Baadhi ya sababu zinazoweza kuhatarisha akaunti yako ni kama wewe:
- Kusambaza taarifa zako binafsi.
- Utumiaji wa wifi ya umma.
Usibonyeze viungo na faili zisizo rasmi.
- Utumiajia wa nenosiri dhaifu.
- Usiweke uthibitishaji wa hatua mbili.
Tafadhali wasiliana na timu yetu ya Msaada kwa Mteja ikiwa una mashaka au wasiwasi.
Tovuti za hadaa mara nyingi huwa na URLs ambazo:
- Zimeandikwa kimakosa.
- Inaanza na HTTP, ambapo inaonyesha si salama (URLs salama huanza na HTTPS).
- Tumia vikoa vya umma ambavyo haviishia na .com, org, au .net.
- Ukosefu wa viashiria vya usalama, kama alama ya kufuli.

Baadhi ya viashiria vya hatari katika barua pepe za hadaa:
- Anwani ya barua pepe ya mtumaji haiishi na @deriv.com.
- Makosa ya tahajia na kisarufi.
- Wanakwambia ubofye viunganishi (link) na viambatisho vinavyotiliwa shaka.
- Ahadi ya kupata pesa kwa urahisi na faida kubwa.
- Maombi ya kuchukua hatua za haraka kama vile kuhamisha pesa zako kwenye akaunti ya benki.

Angalia shughuli za akaunti: makosa ya tahajia kwenye jina la akaunti, uwiano wa kufuatilia na wanaowafuata usio wa kawaida, na ofa zilizojaa emoji ambazo zinaonekana nzuri kupita kiasi ni viashiria vya hatari. Deriv kamwe haiombi taarifa zako binafsi au za kifedha kupitia mitandao ya kijamii, wala hatutoi zawadi/promosheni. Thibitisha akaunti yako kupitia akaunti zetu rasmi za mitandao ya kijamii iliyoorodheshwa chini ya tovuti yetu.
Hapana, usalama wa akaunti yako ni jukumu lako mwenyewe. Unaweza kuangalia baadhi ya mbinu bora za kukaa salama kwenye ukurasa wa kuzuia ulaghai.
Hapana, Deriv haitoi zawadi kwa kuripoti matapeli.
Ikiwa unaamini kuwa umeibiwa taarifa kwa udanganyifu au stakabadhi zako zimevunjwa, ni muhimu kuchukua hatua hizi mara moja ili kulinda akaunti zako za mtandaoni na data zako binafsi:
- Badilisha nenosiri lako: Badili nenosiri la akaunti yako mara moja. Tumia nenosiri thabiti, la kipekee, ambalo linaweza kuzalishwa kwa kutumia zana za usimamizi wa nenosiri.
- Wezesha 2FA: Ikiwa akaunti yako inaweza kutumia uthibitishaji wa hatua mbili (2FA), iwezeshe. Hii hutoa safu ya ziada ya usalama kwa kutoa njia ya pili ya uthibitishaji (m.f., msimbo inaotumwa kwenye simu yako) ili kufikia akaunti yako.
Angalia akaunti zako: Kagua akaunti zako zote za mtandaoni (barua pepe, mitandao ya kijamii, benki, n. k.) ili kuhakikisha hazijadukuliwa pia. Ikiwa unatumia nenosiri moja kwa akaunti nyingi, badilisha nenosiri hilo pia.
- Scani virusi: Fanya uchunguzi kamili wa mfumo kwenye kompyuta yako na vifaa vyovyote ulivyotumia kuingia kwenye akaunti yako. Hakikisha programu yako ya antivirusi na programu ya anti-malware imesasishwa.
- Fuatilia akaunti: Angalia kwa makini akaunti zako kwa shughuli zozote za kutiliwa shaka. Hii inajumuisha kuangalia miamala ambayo haijathibitishwa, mabadiliko kwenye mipangilio ya akaunti, au majaribio mapya ya kuingia kwenye akaunti.
- Arifu Deriv: Wasiliana na timu yetu ya Msaada kwa Wateja. Tafadhali andaa taarifa za akaunti ya tapeli na ushahidi/picha za skrini ili tuweze kuchukua hatua zinazofaa haraka iwezekanavyo.
Hapa kuna hatua chache unazoweza kuchukua mara moja unapogundua miamala isiyotambulika:
- Arifu Deriv: Wasiliana na timu yetu ya Msaada kwa Wateja. Tafadhali andaa taarifa za akaunti ya tapeli na ushahidi/picha za skrini ili tuweze kuchukua hatua zinazofaa haraka iwezekanavyo. Kulingana na uzito wa hali hiyo, huenda tukasimamisha kwa muda au kufunga akaunti yako ili kuzuia miamala mingine isiyoidhinishwa.
- Badilisha nenosiri lako la Deriv: Badili nenosiri la akaunti yako mara moja. Tumia nenosiri thabiti na la kipekee, ambalo linaweza kuundwa kwa kutumia zana za usimamizi wa nenosiri. Ikiwa unatumia nenosiri hili moja kwa akaunti nyingine, hakikisha unabadilisha pia.
- Fuatilia akaunti zako: Angalia kwa makini akaunti zako kwa shughuli zozote za kutiliwa shaka. Hii inajumuisha kukagua miamala isiyoidhinishwa, mabadiliko ya mipangilio ya akaunti, au majaribio mapya ya kuingia kwenye akaunti.









