Ulinzi

Lengo kuu la tapeli ni kuiba taarifa zako muhimu na fedha zako.
Hizi ni baadhi ya njia za kutambua wajifanyao kuwa huduma kwa wateja wa Deriv:
- Wajifanyao wanauliza maelezo yako ya kuingia au taarifa nyingine nyeti kupitia Telegram.
- Wanatoa zawadi zinazoonekana kuwa nzuri mno hivi kwamba haziwezi kuwa za kweli.
- Wanadai malipo kupitia njia zisizoweza kufuatiliwa, kwa mfano, kupitia cryptocurrency.
- Wanakwambia upakue app ambayo haijatolewa kwenye Google Play Store au Apple App Store.
- Wanakwambia upakue programu inayoruhusu kifaa chako kudhibitiwa kwa mbali.
- Wanakwambia upakue faili zenye programu hasidi au virusi vinavyoweza kuathiri kifaa chako.
Bila shaka, orodha hii haijakamilika. Kila siku, matapeli wanakuja na mbinu mpya kujaribu kuiba taarifa zako na pesa.
- Usitoe taarifa za akaunti yako au taarifa zako binafsi kwa mtu yoyote kupitia Telegram.
- Kama kitu kinaonekana kizuri sana kuwa kweli, usikiamini.
- Kamwe usipakue apps kupitia Telegram.
- Kagua file zote kupitia antivirus iliyosasishwa kwanza kabla ya kuzipakua.
- Hakikisha umejiunga na Deriv group sahihi kwenye Telegram.
- Ikiwa umewasiliana na mtu anayeweza kuwa tapeli au kama una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia mazungumzo mubashara.
Mifano ya ujumbe toka kwa matapeli:

Hapa kuna baadhi ya njia za kutambua barua pepe kutoka kwa matapeli:
- Barua pepe imeandikwa vibaya, ina makosa ya kisarufi, na makosa mengi ya tahajia.
- Matapeli watakwambia utume taarifa za siri kupitia majukwaa yasiyo salama, kwa mfano, kupitia SMS, WhatsApp, barua pepe, n.k.
- Wanakwambia ujaze fomu kwenye wavuti isiyosalama bila unganisho la HTTPS (salama).
- Wanakwambia upakue apps za simu zisizo salama katika mfumo wa APK faili ambazo hazitolewi kwenye Google play store au App Store.
- Wanakwambia upakuze viambatisho vya faili au programu za upatikanaji wa mbali (kama Teamviewer) kuwapa udhibiti wa mbali wa kifaa chako. Kwa mfano, tapeli anayeiga anaweza kuchukua udhibiti na kusakinisha programu hatarishi ya ransomware kwenye kifaa chako kisha kudai fidia. Ikiwa fidia haitalipwa, huenda ukapoteza kabisa uwezo wa kufikia kifaa chako.
- Matapeli mara nyingi hutumia vikoa vya barua pepe bila malipo kama @yahoo.com, @gmail.com, au @protonmail.com. Daima soma anwani kamili ya barua pepe ya mtumaji ili kujua ni nani aliyetuma barua pepe hiyo. Kumbuka: Barua pepe kutoka Deriv zitakuja kila mara kutoka @deriv.com.









