Asante! Uwasilishaji wako umepokelewa!
Lo! Kuna kitu kilienda vibaya wakati wa kuwasilisha fomu.

Uwekaji na utoaji pesa

Ni njia gani za malipo ninaweza kutumia kuweka na kutoa pesa?

Unaweza kutumia kadi za debit na credit, e-wallets, cryptocurrency wallets, Deriv P2P, benki mtandao, na fiat onramp kwa kuweka na kutoa pesa. Tazama ukurasa wa njia za malipo kwa orodha kamili.

Mara tu unapoingia kwenye akaunti yako ya Deriv, utaweza kuona njia za malipo zinazopatikana nchini mwako wakati unaposimamia fedha zako.

Je, inachukua muda gani uwekaji na utoaji wangu wa pesa kushughulikiwa?

Tunashughulikia amana na withdrawals zako ndani ya masaa 24 (kutegemea njia yako ya malipo na ukaguzi wa ndani). Inaweza kuchukua muda mrefu kwa fedha zako kufika kwako kutokana na nyakati tofauti za processing kutoka kwa benki na watoa huduma za malipo. Tazama ukurasa wetu wa Njia za Malipo kupata orodha kamili ya muda wa kushughulikia kwa kila njia ya malipo.

Kipi ni kiasi cha chini cha kuweka au kutoa pesa?

Kiasi cha chini cha amana na kutoa kinatofautiana kulingana na njia ya malipo. Kiasi cha chini cha amana na kutoa ni 5 hadi 10 USD/EUR/GBP/AUD kupitia e-wallets. Tazama ukurasa wetu wa Njia za Malipo kupata orodha kamili ya njia za malipo na kiasi cha chini cha kuweka na kutoa fedha.

Hakikisha umeangalia sehemu ya spam au junk katika barua pepe yako pia ikiwa kama hujapokea kiunganishi kwenye sanduku lako la ujumbe.

Ili kuomba kiungo kipya, nenda Hakikisho na bonyeza Thibitisha ombi langu. Tutakutumia kiungo kipya kwa barua pepe, tafadhali kitumie ndani ya saa 1.

Je, ninawezaje kuondoa kikomo cha utoaji kwenye akaunti yangu?

Tutaondoa kikomo cha kutoa USD 10,000 mara tu akaunti yako inapothibitishwa.

Kwa nini nikiweka pesa kwa credit kadi yangu inakataliwa?

Hizi ni baadhi ya sababu kwa nini uwekaji wako kwa kutumia kadi ya credit ulikataliwa:

  1. CVV imefeli. Tafadhali wasiliana na benki yako ili kuangalia.
  2. Kikomo cha kuweka, tafadhali jaribu tena baada ya saa 1-2 ili kuweka.
  3. SCA imefeli. Tafadhali wasiliana na benki yako ili kuangalia.
  4. RCS imekataliwa, idadi inayoruhusiwa ya kadi imezidi. Tafadhali wasiliana na benki yako ili kuangalia.

Ikiwa unahitaji msaada, tafadhali wasiliana nasi kupitia mazungumzo mubashara.

Je, ninaweza kutoa bonasi yangu ya amana?

Ndio, lakini mara tu mauzo yako yanapozidi kiasi ambacho ni mara 25 ya thamani ya bonasi ya amana. Bonasi niya kukusaidia kuyafahamu majukwaa yetu ya biashara, kwa hivyo tunapenda uitumie kufanya biashara na kupata faida inayoweza kutokea (ambayo unaweza kutoa wakati wowote).

Je, unatumia viwango gani vya ubadilishaji kwa kuweka an kutoa pesa?

Mabadiliko ya sarafu kwa amana na uondoaji wako yanafanywa na mpelekaji huduma zako za malipo. Kwa mfano, ukiwa na Skrill, kiasi chako cha muamala kitabadilishwa na Skrill. Tafadhali angalia na mpelekaji huduma zako kuhusu viwango vya kubadilisha vinavyotumika kwa amana na uondoaji wako.

Je, ninawezaje kughairi utoaji wangu pesa?

Ili kughairi kutoa, fuata hatua hizi:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa Utoaji.
  2. Tutakutumia barua pepe ikiwa na kiunganishi cha uthibitishaji. Bonyeza kiunganishi hicho.
  3. Utaelekezwa tena kwenye ukurasa wa Utoaji. Bofya Zinazosubiri ukaguzi kisha uchague muamala ambao ungependa kughairi.
  4. Bonyeza Ndio kuthibitisha kughairi. Fedha zako zitarudishwa kwenye akaunti yako ya Deriv, na salio la akaunti yako litabadilika ipasavyo.

Kumbuka: Huwezi kufuta maombi ya kutoa pesa ikiwa maombi yako tayari yameidhinishwa na kutekelezwa.

Je, ninaweza kuweka pesa kwa kutumia debit/credit kadi za marafiki/familia au e-wallet?

Hapana. Ili kulinda fedha zako, unakatazwa vikali kutumia njia za malipo ambazo si zako. Ikiwa utatumia njia ya malipo ya mtu mwingine, tutasitisha akaunti yako ya Deriv kwa sababu za usalama.

Kwa nini siwezi kuona njia yoyote ya malipo kwenye ukurasa wa kutoa?

Njia yako ya malipo itaonekana tu kwenye ukurasa wa Uondoaji baada ya kufanya amana yako ya kwanza. Iwapo umefanya amana na bado huoni njia yako ya malipo kwenye skrini ya Uondoaji, inahisiwa kuwa njia ya malipo uliyotumia kwa amana haiwezi kutumika kwa uondoaji. Katika hali hii, unaweza kuhitaji kutumia njia tofauti ya malipo inayounga mkono uondoaji pia. Wasiliana nasi kupitia mazungumzo mubashara ikiwa unahitaji msaada.

Je, ninaweza kutumia anwani ya aina moja kuweka cryptocurrency?

Tafadhali tengeneza anwani kwenye ukurasa wa uwekaji wa cryptocurrency wakati wowote unapotaka kuweka pesa. Daima tumia anwani mpya iliyotengenezwa ili kuhakikisha usahihi.

Je, ninaweza kutumia Binance wallet yangu kuweka cryptocurrency?

Unaweza kutumia wallet yoyote kuweka pesa maadamu wallet iwe inaweza kufanya kazi katika njia za mtandao tunazotumia.

Je, kipi ni kiwango cha chini cha kuweka na kutoa kwa cryptocurrency?

Hakulikuwa na kiwango cha chini cha kuweka kwa cryptocurrency. Kiwango cha chini cha kutoa hakijawekwa, kwa hivyo, tafadhali angalia kiasi kwenye ukurasa wa Utoaji.

Je, ninaweza kuhamisha fedha katika akaunti yangu kwenda kwenye akaunti ya mtu mwingine?

Hapana. Uhamishaji wa fedha unaweza kufanyika tu ndani ya akaunti yako mwenyewe.

Samahani, hatukuweza kupata matokeo yoyote na“
Hali tupu
” ndani yake

Bado unahitaji msaada?

Timu yetu ya Msaada wa Wateja inapatikana 24/7. Tafadhali chagua njia unayopendelea ya mawasiliano. Jifunze zaidi kuhusu Utaratibu wetu wa malalamiko.

Ilani ya kuelekeza kwingine

Unaelekezwa kwenye wavuti ya nje.